Bernie Sanders: Trump uongo wake ni wakuzaliwa nao

Bernie Sanders: Trump uongo wake ni wakuzaliwa nao

Bernie Sanders amesema kuwa Rais wa serikali ya Marekani anauongo wa kuzaliwa nao na kusisitiza kuwa wananchi wa Marekani watakabiana naye ipasavyo

Shirika lahabari AhlulBayt (a.s) ABNA: hayo yamesemwa na Bernie Sanders mbunge aliopita katika uchaguzi wa ubunge uliopita siku ya Jumanne na kushika nafasi hiyo katika jimbo la Vermont kwa mara ya tatu mfululizo, ambapo katika hutuba yake baada ya kupata ushindi, Rais wa jamhuri ya Marekani ni katika watu waongo ambao uongo wamezaliwa nao, ama wananchi wa Marekani watakabiliana naye katika hilo.
Aidha ameongeza kusema kuwa moja mbaya ni kwamba tuna Rais katika taifa letu kwamba uongo wake ni waasili, huku akiyafanya mambo ambayo sijawahi kumuona Rais yeyote akiyafanya mambo kama  hayo.
Bernie Sanders amebainisha kuwa Rais wa Marekanni badala ya kuwafanya watu wawe pamoja, daima amekuwa akiwagawa watu kwa rangi, utaifa na imani, huku akibainisha kuwa, wadhifa wetu ni kumuambia Rais huyu,  hakika tumechoka na siasa za ubaguzi nchini Marekani.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

We are All Zakzaky