Erdogan aapishwa na kuanza muhula mpya wa uraisi nchini Uturuki

Erdogan aapishwa na kuanza muhula mpya wa uraisi nchini Uturuki

Muhula mpya wa urais wa jamhuri ya Uturuki “Erdogan” waanza leo baada ya kufanyika sherehe za kumuapisha katika bunge la nchi hiyo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: kuanza kwa muhula huo ni baada tu ya kuapa kwake katika Bunge la nchi hiyo, alkadhalika baada ya kuapa kwake pia amebadili muundo wa utawala wa nchi hiyo kutoka katika Bunge hatimaye kuwa na mfumo wa Rais.
Wananchi wa Uturuki mwanzoni mwa mwaka uliopita walipiga kura ya kubadili muundo wa serikali ya nchi hiyo, kutoka muundo wa usimamizi wa Bunge na kwenda katika usimamizi wa Rais, ambapo baada ya hapo Rajab Tayyip Erdogan ndiye Rais wa kwanza katika mfumo mpya huo.
Aidha sherehe za kuanza utawala mpya zilifanyika kwa kuhudhuriwa na wageni waalikwa kutoka mataifa 50 nchini humo, ambapo kwa ujumla sherehe hizo zimehudhuriwa na wageni waalikwa elfu 6 kutoka ndani na nje ya Uturuki.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Prophet's birthday celebrations
We are All Zakzaky