Kauli mbiu za kuleta mfaraka zakatazwa kwa shiriki maombolezo katika mji wa Karbala

Kauli mbiu za kuleta mfaraka zakatazwa kwa shiriki maombolezo katika mji wa Karbala

Kamanda mkuu wa jeshi la Polisi mjini Karbala ametoa kauli na ujumbe kwamba wa kutangaza kuwa, hairuhusiwi kwa waombolezaji kutumia kauli mbiu zitakazoleta mitafaruku baina ya waombolezaji katika mji huo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: hayo yamesemwa na kamanda mkuu wa jeshi la Polisi katika mkoa wa Karbala na kuashiria kuwa, mpango kamili wa usalama wa waombolizaji wa masaiabu ya Imamu Husein (a.s), umeandaliwa ipasavyo kwaajili ya kuhakikisha usalama na amani wa waombolezaji unapatikana.
Aidha akibainisha suala hilo amesema: maeneo yote ya mkoa wa Karbala yameanishwa barabara ya magari kuingia na kutoka katika maeneo ya mji Huo ikiwepo magari ya zimamoto, alkadhalika maeneo ya kupita waombolezaji katika muda wote wa maombolezo ya mauaji ya kikatili ya mjukuu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) katika m,ji huo, hivyo tunawataka waombolezaji wote kujiepusha na kauli mbiu zitakaoleta uchochezi na mtafaruku baina ya waombolezaji.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni