?>

Mahakama ya kimataifa yalipokea shtaka la Iran dhidi ya Marekani

Mahakama ya kimataifa yalipokea shtaka la Iran dhidi ya Marekani

Mahakama ya umoja wa Mataifa imetangaza rasmi kulipokea shtaka la Iran dhidi ya serikali ya Marekani

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: mahakama ya kimataifa (ICJ) yadhipitisha kupokea mashtaka ya Iran dhidi ya utawala wa Marekani ambao umepanga kurejesha vikwazo kwa Iran kwa mara nyingine.
Hayo yametolewa katika ujumbe ulisambazwa na mahakama hiyo na kusisitiza kuwa: jamhuri ya kiislamu ya Iran imefikisha shitaka lake dhidi ya Marekani katika mahakama ya umoja wa Mataifa ikiwa moja wapo ya sehemu za kutaka sheria ichukue nafasi yake, mashtaka hayo ni pamoja na Marekani kuto tekeleza mikataba ya kibiashara na mengineyo baina ya Marekani na Iran.
Rais wa Marekani tarehe nane mwezi Mei mwaka huu alijitoa katika makubaliano ya mpango wa Nyuklia wa Iran bila ya sababu za msingi, na kutishia kuwa atarejesha vikwazo vyote ambavyo aliwekewa Iran.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*