Makumi ya majeshi ya Sudan yaangamia nchini Yemen

Makumi ya majeshi ya Sudan yaangamia nchini Yemen

Majeshi ya Yemen syametangaza kuuwawa kwa makumi ya wanajeshi wa Sudan nchini Yemen katika mkoa wa Hujjeh nchini humo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: majeshi ya Yemen yanayoshirikia na kikundi cha Ansarullah yametangaza kuuwawa kwa makumi ya majeshi ya mamluki wa Saudi Arabia waliotumwa nchini Yemen, baada ya kuingia katika mtego waliotegewa na majeshi ya Yemen katika mkoa wa Hujjeh.
Kwa mujibu wa ripoti hii, mashambulizi ya yaliofanywa dhidi ya majeshi hayo yamepelekea luangamia kwa makumi ya wanajeshi hao wamekufa na kujeruhiwa, huku wakifanikiwa kuteka magari kadhaa ya umoja wa majeshi ya kuivamia Yemen chini ya usimamizi wa utawala wa Saudi Arabia.
Inasemekana kwamba Sudan ni moja kati ya mataifa yalioshiriki katika umoja wa kuivamia kijeshi Yemen, ambapo utawala wa Saudi Arabia toka miaka mitatu iliopita imevamia kijeshi Yemen ikishirikiana na mataifa kadhaa ya kiarabu dhidi ya taifa hilo.
Toka kipindi hicho mpaka leo uvamizi huo umepelekea kuawawa kwa maelfu ya wananchi wasiokuwa na hatia na wengine wengi kujeruhiwa, huku miundombinu ya taifa hilo ikihariiwa.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni