Mamilioni ya waislamu wahudhuria ibada ya hijja

Mamilioni ya waislamu wahudhuria ibada ya hijja

Zaidi ya Waislamu milioni mbili kutoka duniani kote wamehudhuria ibada ya hija katika maeneo takatifu ya Kiislamu nchini Saudi Arabia.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Zaidi ya Waislamu milioni mbili kutoka duniani kote wamehudhuria ibada ya hija katika maeneo takatifu ya Kiislamu nchini Saudi Arabia.

Hija ni mkusanyiko wa pili unaokusanya waislamu wengi baada ya mkusanyiko wa arobaini ya Imam Husein mjukuu wa mtume ambaye aliuawa kikatili katika mji wa Karbala. Kusanyiko wa Karbalaa hupokea waislamu zaidi ya milion 10 kila mwaka.

Nchi hiyo ya kifalme ambayo ni ya kihafidhina zaidi, na ambayo inafanya mageuzi makubwa ya kijamii na kiuchumi, imekusanya raslimali nyingi kwa ajili ya kufanikisha ibada hiyo ya  siku sita, ambayo ni mojawapo ya nguzo tano za Uislamu.

Pamoja na kwamba kipindi hiki ni kitukufu kwa waislam, majeshi ya Saudia arabia yakiongozwa na Marekani na kushirikiana na majeshi ya kiarabu wanaendela kufanya mauaji ya kutisha dhidi ya wananchi wa Yemen.

Wakati huo huo, Qatar imeilaumu Saudi Arabia kwa kuwazuia raia wake kuhudhuria hija ya mwaka huu kutokana na mzozo wa kidiplomasia unaoendelea kati ya nchi hizo mbili. Serikali ya Saudi Arabia hata hivyo imekanusha hayo na kusema Waqatari bado wanasafiri kuelekea Mecca.

Katika mpango wa kuzuia idadi kubwa ya Waqatari kuingia nchini humo Saudi Arabia ilikuwa imewakubalia Waqatari 1,200 pekee kuhudhuria hija ya mwaka huu ila Qatar inasema raia wake hawajaweza kupata vibali vya kuingia

Qatar inalaumu suala hilo kutokana na mzozo wa kidiplomasia na majirani zake wa Ghuba - Saudi Arabia, nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu, Bahrain na Misri. Shirika la kutetea haki za binadamu la Qatar limesema Saudi Arabia iliufunga mfumo wa kuwasajili watu kielektroniki ambao unatumiwa na mashirika ya usafiri kupata vibali kwa mahujaji wa Qatar. Afisa wa Saudi Arabia amekanusha madai hayo na kuilaumu Qatar akisema wao ndio waliozuia  njia  hiyo ya usajili.

Afisa mmoja wa Wizara ya masuala ya hija wa Qatar amesema kuwa kundi la mahujaji wa Qatar wamewasili Mecca, ijapokuwa hajasema ni wangapi au kama walisafiri moja kwa moja kutoka Qatar. Mwaka jana, zaidi ya mahujaji 1,600 wa Qatar walihudhuria hija.

Bei za mafuta na umeme zinazoongezeka zimewaathiri vikali Wamisri, na kuwalazimu wengi kuchelewesha hadi wakati usiojulikana mipango yao ya sarafi za kuhudhuria ibada ya kila mwaka ya hija.

Mwaka jana, Wamisri 80,000 walifunga safari kwenda Macca lakini maafisa wanasema wanatazamia idadi yam waka huu kupungua kwa asilimia 20, ambapo Wamisri 64,000 wanatarajiwa kuhudhuria.

Mwisho wa habari / 291

 


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

We are All Zakzaky