Marekani yawazuia wapalestina kudai haki zao

Marekani yawazuia wapalestina kudai haki zao

Marekani inatazamiwa kutangaza hatua kali dhidi ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) endapo itawachunguza tuhuma dhidi ya wanajeshi wa Marekani wanaotuhumiwa kufanya uhalifu wa kivita na wakati huo huo itaufunga ubalozi wa Palestina mjini Washington.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Marekani inatazamiwa kutangaza hatua kali dhidi ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) endapo itawachunguza tuhuma dhidi ya wanajeshi wa Marekani wanaotuhumiwa kufanya uhalifu wa kivita na wakati huo huo itaufunga ubalozi wa Palestina mjini Washington.

Mshauri wa masuala ya usalama wa Rais Donald Trump, John Bolton, alitazamiwa kuweka bayana hayo kwenye hotuba yake ya mchana wa jana Jumatatu  tarehe 10 Septemba 10, wakati akizungumza na kundi la kihafidhina lijiitalo Federalist Society mjini Washington.

Kwa mujibu wa rasimu ya hotuba hiyo, Bolton angeliuwambia mkutano huo kuwa Marekani itatumia kila njia ili kuwalinda raia wake na wa washirika wake waliofanya makosa dhidi ya kile anachokiita "mashitaka yasiyo ya haki ya mahakama isiyo halali". 

Endapo uchunguzi huo utaanzishwa na ICC, utawala wa Trump utafikiria kuwapiga marufuku majaji na waendesha mashitaka wa mahakama hiyo ya kimataifa kuingia nchini Marekani, na pia utazizuwia fedha zote walizonazo ndani ya mfumo wa kifedha wa Marekani, sambamba na kuwafungulia mashitaka kwenye mahakama za Marekani.

"Hatutashirikiana na ICC, hatutaipa msaada, hatutajiunga nayo. Tutaiwacha ife yenyewe. Tangu hapo kwa dhamira na dhati yake, ICC kwetu sisi tayari imeshakufa!" Inasema sehemu ya hotuba hiyo.

Ofisi za PLO Washington kufungwa

Kwenye hotuba hiyo pia, Bolton alitarajiwa kubainisha mipango ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani kuifunga ofisi ya Chama cha Ukombozi cha Palestina (PLO) mjini Washington, kutokana na wasiwasi kwamba Palestina inajaribu kuiomba  mahakama ya jinai za kivita ICC ichunguze mauaji ya kinyama yanayofanywa na  Israel dhidi ya wapalestina.

Hata hivyo, viongozi wa Palestina walisema hawako tayari kuacha juhudi zao za kuifikisha Israel mbele ya mahakama hiyo ya kimataifa ya uhalifu, wakiuelezea mpango huu wa kuzifunga ofisi za chama chao mjini Washington kuwa ni mbinu ya karibuni kabisa ya utawala wa Trump. 

Marekani Tayari imeshakata ufadhili wake kwenye Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) pamoja na hospitali za Jerusalem Mashariki, eneo ambalo ni mji mkuu wa Palestina lakini unakaliwa kwa mabavu na waisrael wakisaidiwa na mataifa ya Marekani na mataifa ya kiarabu na Magharibi.

Saeeb Erakat, afisa wa ngazi za juu kwenye serikali ya Palestina, alisema kwamba haki za Wapalestina haziwezi kuchuuzwa mnadani na kwamba kamwe hawatatishika kwa vitisho vya Marekani. 

Erakat aliapa kuwa wataiandikia ICC kuitaka ianzishe mara moja dhidi ya uhalifu wa Israel kwenye ardhi ya Wapalestina.

Wakati hayo yanajiri Iran ambayo ndio msaada mkuu kwa wapalestina imeendela kusisitiza kwamba haki za wapalestina zinatakiwa kupatikana hata kwa kutumia nguvu.

Mwisho wa habari / 291

 

 

 


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

We are All Zakzaky