Mkuu wa umoja wa mataifa atoa amri ya kuchunguzwa mauaji ya wanafunzi nchini Yemen

Mkuu wa umoja wa mataifa atoa amri ya kuchunguzwa mauaji ya wanafunzi nchini Yemen

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa ametoa amri ya kufanyika uchunguzi wa haraka kuhusu jinai ziliofanywa dhidi ya wanafunzi nchini Yemen katika mkoa wa Saadah nchini humo

Shirika la habari AhlulaBayt (a.s) ABNA: hayo yamesemwa na katibu mkuu wa umoja wa Mataifa alipokuwa akitoa tamko lake la kupinga mauaji yaliofanywa na ndege za Saudi Arabia kushambulia Basi liliokuwa limebeba wanafunzi watoto katika mkoa wa Saadah, jambo liliopelekea kuuwawa na kujeruhiwa zaidi ya wanafunzi 100 katika shambulio hilo.
Msemaji mkuu wa umoja wa mataifa naye amesema katika kauli hiyo kuwa kiongozi mkuu wa umoja wa mataifa amepinga vikali mauaji hayo yaliofanywa na umoja wa nchi za Kiarabu ukisimamiwa na utawala wa Saudi Arabia na kutaka kufanyika uchunguzi wa haraka katika suala hilo.
Katika kauli hiyo katibu mkuu wa umoja wa mataifa amesisistiza kwa kusema kuwa pande mbili hasimu zinapaswa kuhifadhi maisha ya watoto wasiokuwa na hatia na kuto washambulia watu wa aina hiyo.
Ndege za Saudi Arabia siku ya Alhamisi zilishambulia Basi liliobeba wanafunzi katika mkoa wa Saadah nchini Yemen ambapo ripoti za awali zinaashiria kuuwawa kwa wanafunzi 50 na wengine 77 kujeruhiwa.
mwesho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

We are All Zakzaky