Mmoja kati ya waandamanaji auwawa kwakupigwa risasi mjini Abuja Nigeria+ picha

Mmoja kati ya waandamanaji auwawa kwakupigwa risasi mjini Abuja Nigeria+ picha

Waandamanaji wanaomuunga mkono Sheikh Zakzaky mjini Abuja mji mkuu wa Nigeria washambuliwa na jeshi la Polisi na kupelekea kutokea vujo na kusababisha kuuwawa kwa mmoja kati ya waandamanaji hao

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: mmoja kati ya watu waliokuwa wameshiriki katika maandamano ya amani ya kumuunga mkono Sheikh Zakzaky ameuwawa kwa kupigwa risasi na jeshi la polisi la nchi hiyo.
Maandamano hayo yaliofanyika leo siku ya Jumatano ambayo yaliandaliwa na taasisi ya harakati ya Kiislamu ya Nigeria katika mkoa wa Abuja, mji mkuu wa Nigeria ambapo walishiriki mamia ya wananchi wa nchi hiyo na kabla ya kuisha kwa maandamano hayo ya amani yalivamiwa na jeshi la Polisi hatimaye kutokea vurugu.
Kwa mujibu wa ripoti zilizotufikia ni kwamba jeshi la Polisi katika kuwatawanya waandamanaji hao halikutumia mabomu ya machozi pekee bali lilitumia pia risasi za kivita ambazo zimepelekea kuuwawa kwa muandamanaji mmoja nchini humo.
Katika maandamano hayo ya amani, lengo lake ni kuitaka serikali ya Nigeria kumuachia huru kiongozi wa Taasisi ya harakati ya Kiislamu nchini humo aliokuwa amekamatwa miaka miwiliopita iliopita.

mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

We are All Zakzaky