Muumini na muadhini wa msikiti achinjwa nchini Algeria+ picha

Muumini na muadhini wa msikiti achinjwa nchini Algeria+ picha

Baada ya siku tano ya kuingia mwezi mtukufu wa Ramadhani nchini Algeria muumini mmoja ambaye alikuwa muadhini wa msikiti mmoja nchini humo ameonekana amekatwa kichwa

Shirika la habari AhlulaBayt (a.s) ABNA: muumini mmoja ambaye pia alikuwa ni muadhini wa msikiti mmoja wa sehemu ya Oued Sebaa katika wilaya ya Sidiybalbasi magharibi mwa Algeria apoteza maisha kwa kuchinjwa na watu wasiofahamika siku ya tano ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Aidha kwa mujibu wa ripoti ziliotolewa na vyombo vya habari rasmi vya Algeria kutoka katika vyombo vya uslama vya nchini hiyo kuwa: vyombo vya usalama vya nchi hiyo siku Jumatatu ya tarehe 21 ya mwezi wa tano waliiona miili miwili ya watu waliouliwa katika msikiti wa Khalid bin Walid wa sehemu ya Oued Sebaa, ambapo uchunguzi unaonyesha kuwa miili hiyo ni ya mtu mmoja aliyekuwa muadhini wa msikiti huo mwenye umri wa miaka 64 na mwingine ni muumini aliokuwa akisali katika msikiti huo, ambao waliuliwa baada ya sala ya Alfajiri.
Vyombo vya ulinzi na usalama nchini humo vinaendelea kufanya uchunguzi wa kujua sababu ziliosababisha kutokea kwa mauaji hayo ya kinyama na kuwakamata waliohusika na tukio hilo.
Tukio hilo limeingiza khofu kubwa kwa wananchi na Maimamu wa misikiti mbalimbali nchini humo wanapo kuwa misikitini hata wanapokuwa nje ya misikiti, khofu ambayo imepelekea kufanya maandamano makubwa ya kupinga mauaji hayo.

   
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

We are All Zakzaky