Qatar yazuia kuuza na kununua bidhaa za Saudia, Bahrain, Misri na Emirates

Qatar yazuia kuuza na kununua bidhaa za Saudia, Bahrain, Misri na Emirates

Wizara ya uchumi na biashara nchini Qatar imezuia rasmi kuuza na kununua bidhaa zilio tengenezwa katika nchi za Saudi Arabia, Emirates, Misri na Bahrain katika vituo vyote vya biashara nchini humo

Shirika la habri AhlulBayt (a.s) ANA: waziri wa uchumi na biashara wa Qatar amezitaka sekta zote za biashara na uchumi kuacha kuuza na kununua bidhaa zozote zinazozalishwa Saudi Arabia, Emirates, Bahrain na Misri.
Aidha amesisitiza kwamba kutakuwa na wachunguzi wakipita kila sehyemu za biashara kuchunguza utekelezaji wa amri hiyo ambapo yeyote atakaye kamatwa akiuza bidhaa hizo, hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Wiki iliopita msemaji wa wizara ya mambo ya nje nchini Qatar ameashiria kuwa: Qatar imefanikiwa kushinda katiuka mapambano yake ya kukabiliana na vikwazo waliokuwa wamewekewa na Saudi Arabia, Emirates, Bahrain na Misri dhidi ya nchi hiyo.
Saudi Arabia, Bahrain, Misri na Emirates tarehe tano mwezi wa sita mwaka jana zilikata fungano na Qatar kwa madai kuwa inasaidia ugaidi, hivyo walifunga mawasliano ya kila pande na kufunga mipaka yote.  
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

We are All Zakzaky