Rais wa Uturuki alipomjibu Trumpo usiitishia Uturki

Rais wa Uturuki alipomjibu Trumpo usiitishia Uturki

Rais wa jamhuri ya Uturuki amemuambia Rais wa Marekani, hupaswi kuitishia Uturuki

Shirika la habari Ahlulbayt (a.s) ABNA: Rais wa jamhutri ya Uturuki “Rajabu Tayyip Erdogan” amemuambia Rais wa Marekani kuwa hapaswi kuitishia Uturuki badala yake azungumze naye kwa ludha ya Sheria na makubaliano.
Rais wa Uturuki aliyasema hayo katika hutuba yake aliotoa katika moja ya mikoa ya Uturuki huku akiashiria kuwa mwenendo wa Rais wa Marekani kuhusu Uturuki ni wakuihujumu Uturuki, nasi hatukubali mwenendo huo kwa maana tutaendelea kubaki misingi ya kisheria hivyo hatuogopi vitisho.
Aidha aliendelea kubainisha kuwa: Trumpo anazungumza nasi kwa lugha ya vitisho, lakini afahamu kuwa kamwe Uturuki haitasambaratika kwa kutumia lugha ya vitisho.
Ilitokea hali ya kutoelewana kati ya Uturuki na Marekani baada ya Uturuki kumkamata Padri ambaye ni mwananchi wa Marekani aliyekuwa anajihusisha na ugaidi na kufanya ujasusi dhidi ya Uturuki katika kikundi cha PKK, ambapo serikali ya Uturuki imeahidi kumuhumu Padri huyo nchini hum, jambo ambalo serikali ya Marekani halikubaliani nalo. Mwisho alimalizia kwa kusema kuwa sistimu ya mahakama ya Uturuki ni sistimu huru, hivyo haitafuata matakwa ya serikali ya Marekani.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

We are All Zakzaky