Shambulio la kigaidi dhidi ya Gwaride la jeshi la Iran katika mji wa Ahwazi 25 wauwawa

 Shambulio la kigaidi dhidi ya Gwaride la jeshi la Iran katika mji wa Ahwazi 25 wauwawa

Tukio hilo la kusikitisha limetokea asubuhi ya Jumamosi ya jana ambapo watu walishambulia kwa Rasasi Gwaride liliokuwa linafanywa na Jeshi la Iran katika mkoa wa Ahwazi na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 25 na wengine wengi kujeruhiwa

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: maonyesho ya Gwaride yaliofanywa na jeshi la Iran katika mji wa Ahwazi yameshambuliwa na magaidi ambao walikuwa wamejificha katika Paki iliokuwa nyuma ya jukwaa na uwanja wa kufanyia Gwaride ambapo baada tu ya kuanza kwa Gwaride hilo walianza kuwafyatulia Risasi wanajeshi na wananchi waliohudhuria kuangalia Gwaride hilo.
Aidha wamesema kuwa kufuatia shambulio hilo watu 25 wamepoteza maisha na wengine zaidi ya 57 wamejeruhiwa, huku ikibainishwa kuwa kutokana na majeruhi hao kuwa na hali mbaya zaidi, kuna uwezekano wa kuongezeka kwa idadi ya vifo hivyo.
Ama hatima ya magaidi hao ni kama ifuatavyo kwamba watatu wameuliwa na mmoja amejeruhiwa na kukamatwa na viombo vya usalama vya Iran.


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

We are All Zakzaky