Uturuki: sitasitisha fungamano langu na Iran kwa amri ya mataifa mengine

Uturuki: sitasitisha fungamano langu na Iran kwa amri ya mataifa mengine

Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki amesema: serikali ya Uturuki haitaridhia kuvunja fungamano lake la kibiashara na Iran kwa amri za mataifa mengine

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: hayo yamesemwa na waziri wa mambo ya nje wa Uturuki “Mevlut Cavusoglu” kwa Uturuki kamwe haitaacha fungamano lake la kibiashara na Iran kwa kuamrisha na mataifa mengine ya nje.
Aidha alijibu alipoulizwa na waandishi wa habari wa televishen ya NTV ya Uturuki, akibainisha kuwa serikali ya Marekani imejitoa katika makubaliano ya mpango wa Nyuklia wa Iran, ama umoja wa Ulaya bado ni wenye kufungamana na makubaliano ya mpango wa nyuklia wa Iran, huku akisisitiza kuwa, serikali ya marekani imefanya kosa kubwa sana kutoka katika makubaliano hayo, jambo ambalo sisi hatukunbaliani nalo kwani Iran ni miongoni mwa mataifa makubwa muhimu ambao pia ni majirani zetu.
Kauli hiyo wa waziri huyo wa mambo ya nje wa Uturuki imetolewa baada ya serikali ya Marekani kuyataka mataifa mbalimbali kuacha kununua bidhaa za Iran ikiwemo mafuta.  
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Prophet's birthday celebrations
We are All Zakzaky