Vungamano la Iran na Morocco lasambaratika

Vungamano la Iran na Morocco lasambaratika

Serikali ya Morocco yavunja mahusiano na Serikali ya Iran kwa kile walichokidai kuwa Iran inaunga mkono kikundi cha Polisario front

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: Serikali ya Morocco yavunja mahusiano na Serikali ya Iran kwa kile walichokidai kuwa Iran inaunga mkono kikundi cha Polisario front.
Waziri wa mambo ya nje wa Morocco akithibitisha habari hiyo amesema: tumefunga ubalozi wetu mjini Tehran alkadhalika baada ya muda tutamfukuza balozi wa Iran aliopo nchini. Ama mpaka hakuna ripoti kamaili kuhusu suala hili bado hazipo mikononi mwetu.
Inasemekana kuwa kikundi cha Polisario Front, ni kundi ni kikundi cha kisiasa ambapo kilianzishwa na wananchi kwaajili ya kuzitoa nchi za tawala wa Kifalme za kaskazini mwa Afrika ambapo bado wanaendelea kufanya mapambano katika maeneo hayo.
Kikundi hicho kinadai kuwa maeneo ya kaskazini mwa Afrika kinadai kuwa maeneo hayo ni miliki ya waafrika wazalendo wa sehemu hizo, ambapo walipambana na serikali ya Morocco ambapo mnamo mwaka 1991 walisitisha vita chini ya usimamizi wa umoja wa mataifa, ama hivi sasa bado matatizo baina ya kikondo hicho na serikali ya Morocco.

mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

We are All Zakzaky