wanajeshi 180 wanaongozwa na Saudi Arabia wapoteza na kujeruhiwa nchini Yemen

wanajeshi 180 wanaongozwa na Saudi Arabia wapoteza na kujeruhiwa nchini Yemen

msemaji mkuu wa majeshi ya Yemen ametangaza kuwa majeshi ya umoja wa waarabu chini ya uongozi wa Saudi Arabia yamepata kipigo kikali katika mashambulizi yaliotokea katika Bandari ya Hudaydah nchni Yemen

shirika la habari AhluLbayt (a.s) ABNA: katika masaa 48 yaliopita zaidi ya watu 100 miongoni mwa majeshi ya umoja wa waarabu katika kuivamia Yemen ukiongozwa na Saudi Arabia, katika mashambulizi makali yaliotoka sehemu ya Hudaydah nchini Yemen.
Hayo yamesemwa na Yahya Sariu, msemaji rasmi wa majeshi ya Yemen kwamba: majeshi yanayoongwa na Saudi Arabia nchini Yemen katika masiku mawili yaliopita kufuatia mashambulizi makali, yamepata hasara kubwa kwa kupoteza majeshi yao na kuangamizwa kwa vifaa vya kivita vya majeshi hayo yanaosimamiwa na Saudi Arabia.
Aidha aliongeza kusema kuwa zaidi ya wanajeshi 180 wameuwawa na kujeruhiwa kufuatia mashambulizi hayo, ambapo miongoni mwa waliopoteza maisha ni pamoja na makamanda kumi wa majeshi hayo.
Msemaji huyo amesema kuwa kufuatia ripoti hii ni kwamba makumi ya miili pamoja na majeruhi imeamishiwa katika Hospitali ya “Al-Makha” nchini humo.

mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

We are All Zakzaky