Watu kadhaa wajiruhiwa kwa silaha baridi nchini Finland+ picha

Watu kadhaa wajiruhiwa kwa silaha baridi nchini Finland+ picha

Mtu moja aliokuwa na kisu amewajeruhi watu kadhaa katika mji wa Durga nchini Finland

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) jeshi la Polisi nchini Finland lemetangaza kuwa watu kadhaa wamejeruhiwa kwa kisu katika mji wa Durga nchini Finlan, ambapo muhusika aliofanya tukio hilo pia  ametiwa mbaroni.
Kwa mujibu wa ripoti shirika la habari la Reuters ni kwamba mtu aliokuwa na kisu aliwashambulia watu kadhaa na kuwajeruhi vibaya nchini humo.
Aidha jeshi la Polisi la Finland limeeleza kuwa, mshambuliaji wa tukio hilo amefanya shambulio hilo kwa kisu na kusababisha kujeruhiwa watu kadhaa upande wa kusini mwa mji wa Durga nchini humo.
Baada ya kutokea tukio hilo, jeshi la Polisi nchini humo limeimarisha ulinzi zaidi katika viwanja vya ndege vya nchi hiyo, kwa upande mwingine wamefanikiwa kumtia mbaloni mtuhumiwa huyo.
Jeshi la Polisi limewaambia wananchi wa mji huo kuwa wajiepushe kwenda katika makao makuu ya mji huo, huku picha ziliosambazwa kuhusu tukio hilo zinaonesha, mmoja kati ya majeruhi amelazwa chini akiwa amefunikwa shuka katika moja ya midani za mji huo ziliopo katika makao makuu ya mji hio.
Ama jeshi mpaka sasa halijathibitisha kufariki kwa yeyete kati ya wahanga wa tukio hilo.


mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni