Wazayuni 42 wajeruhiwa kufuatia shambuli la makombora ya Hamas

Wazayuni 42 wajeruhiwa kufuatia shambuli la makombora ya Hamas

Vyombo vya habari vya kizayuni vimetanga kujeruhiwa kwa wazayuni 42 kufuatia mashambulio ya makombora ya majeshi ya Hamas katika vitongoji viliojengwa kwa nguvu na utawala haramu wa Israel

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: vyombo vya habari vya kizayuni vimetoa ripoti kuwa usiku wa Jumatatu vikosi vya Hamas vilifanya mashambulizi makali katika maeneo yanayokaliwa kwa nguvu na wazayuni hao na kupelekea kujeruhiwa zaidi ya wazayuni 46 sehemu hiyo.
Majeshi ya kikundi kinachopambana dhidi ya utawala haramu wa Israel, kimefanya mashambulizi kwa makombora katika maeneo yaliokaliwa na wazayuni kwa nguvu katika ukanda wa Gaza nchini Palestina
Aidha usiku wa Jumatatu Hamas walirusha zaidi ya Roketi 100 na makombora mengine kutoka ukanda wa Gaza kwenda katika vitongoji vilivyojengwa kwa nguvu na utawala haramu wa Israel viliokaribu na ukanda wa Gaza.
Vyanzo makini vya utawala haramu wa Israel umesisitiza kuwa shambulio la Roketi za kikundi cha Hamas zimesambaratisha Basi moja katika vitongoji hivyo, huku vikundi vya Hamas nchini Palestina vimetangaza kuwa mashambulizi ya Roketi hizo ni majibu ya mauaji ya wanajeshi saba wa kikundi hicho wauwawa katika shambulio liliofanywa na majeshi ya Israel katika ukanda wa Gaza.

mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

We are All Zakzaky