Zaidi ya wanajeshi 60 wa Saudi Arabia wajiuzulu kufuatia vita ya Yemen

Zaidi ya wanajeshi 60 wa Saudi Arabia wajiuzulu kufuatia vita ya Yemen

Mmoja miongoni mwa wana harakati wa habari kupitia Twitter nchini Saudi Arabia ametangaza taarifa za maficho katika familia ya kifalme nchini humo kuwa wanajeshi wapatao 60 wamejiuzulu kazi hiyo kufuatia vita inayoendelea nchini Yemen

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: mwana harakati hiyo maarufu nchini Saudi Arabia kwa jina la (Mujtahid) katika habari zake mpya amefichua habari hii kuwa zaidi ya wanajeshi 60 wenye vyeo mbali mbali katika jeshi la nchi hiyo, wamewasilisha barua ya kujiuzulu na nafasi hizo nchini humo.
Aidha ameendelea kusema kuwa sababu ya msingi ya kujiuzulu huko ni kile walichokisema kuwa wanahisi kukiuka ubinadamu kuhusu yale yanatokea nchini dhidi ya wananchi wa Yemen, huku wakiwa na hofu ya kuwekwa majina yao kuwa miongoni mwa watu waliofanya jinai dhidi ya ubinadamu.
Kadhalika amebainisha kuwa utawala wa Saudi Arabia mpaka sasa hujaafiki na kupitisha maombi ya kujiuzulu huko, ambapo kwa upande mwengine wanajeshi hao hunekana kuwa wamefanya kosa la jinai kwa mtazamo wa serikali ya Saudi Arabia.

mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

We are All Zakzaky