Gaidi mkubwa wa Al-shabab aangamizwa nchini Somalia

Gaidi mkubwa wa Al-shabab aangamizwa nchini Somalia

Mmoja miongoni mwa magaidi wakubwa wa kikundi cha kigaidi cha Al-shabab nchini Somalia ameangamizwa na kuuliwa nchini humo, baada ya kuingia katika mtego aliotegewa na majeshi ya umoja wa Afrika.

Shirikala habari AhlulBayt (a.s) ABNA: kamanda mkuu wa majeshi ya umoja wa Afrika nchini Somalia ametangaza kuwa wamefanikiwa kummaliza mmoja kati magaidi wakubwa wa kikundi cha kigaidi cha Al-shabab nchini Somalia, ambapo gaidi huyo aliengia katika mtego wa majeshi ya Umoaja wa Afrika katika kijiji Barbariy nchini humo.
Kikundi cha kigaidi cha Al-shabab ni katika vikungo vya siasa kali vyenye kufanya mauaji dhidi ya watu wasiokuwa na hatia kilianza kufanya mauaji nchini Somalia mnamo mwaka 2012 ambapo kikundi hicho kinasadikiwa kuwa ni wafuasi wa kikundi cha kigaidi cha Al-qaida.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

We are All Zakzaky