Watu 10 wauawa katika shambulizi Shuleni Marekani

Watu 10 wauawa katika shambulizi Shuleni Marekani

Marekani imekumbwa na mauaji mengine ya bunduki shuleni. Mara hii mshambuliaji ameilenga shule ya mjini Santa Fe mjini Texas, akiuwa watu 10, wengi wao wanafunzi.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Marekani imekumbwa na mauaji mengine ya bunduki shuleni. Mara hii mshambuliaji ameilenga shule ya mjini Santa Fe mjini Texas, akiuwa watu 10, wengi wao wanafunzi.

Watu 10, wengi wao wakiwa wanafunzi wameuawa na mshambuliaji mwenye bunduki kwenye shule moja ya mjini Santa Fe, katika jimbo la Texas nchini Marekani. Muuaji ametambuliwa kuwa ni mwanafunzi mwenye umri wa miaka 17 aitwaye Dimitrios Pagourtzis, na tayari amefunguliwa mashitaka ya mauaji akikabiliwa na adhabu ya kifo.

Gavana wa Texas Greg Abbot ameyaita mauaji hayo tukio baya kabisa katika historia ya shule jimboni humo, na kuthibitisha kuwa bunduki mbili alizotumia muuaji huyo zilikuwa zikimilikiwa kihalali na baba yake. Hata hivyo, gavana huyo hakulaumu umiliki holela wa bunduki, badala yake amejikita juu ya haja ya kushughulikia matatizo ya kiakili.

Jioni ya jana mamia ya watu, miongoni mwao wakiwemo watoto, walibeba mishumaa kuomboleza waliouawa. Yamekuwepo mashambulizi 22 ya bunduki katika shule nchini Marekani tangu kuanza kwa mwaka huu wa 2018.

Mwisho wa habari / 291


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

We are All Zakzaky