?>

Hali mbaya ya haki ya kusema na kujieleza Uingereza yatia wasiwasi

Hali mbaya ya haki ya kusema na kujieleza Uingereza yatia wasiwasi

Matokeo ya uchunguzi wa maoni uliofanyika hivi karibuni yanaonyesha kuwa, nusu ya wananchi wa Uingereza wanaamini kuwa, uhuru wa kusema na kujieleza unakabiliwa na hatari nchini humo.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Uchunguzi wa maoni uliofanywa na gazeti la Daily Telegraph unaonyesha kuwa, asilimia 50 ya Waingereza wanaamini kuwa uhuru wa kusema na kujieleza nchini humo unakabiliwa na hatari.

Uchunguzi huo unaonyesha kuwa, asilimia 12 ya Waingereza wanaitakidi kuwa kiwango cha uhuru wa kusema nchini humo kimeboreshwa ikilinganishwa na miaka mitano iliyopita na asilimia 49 miongoni mwao wanaamini kinyume chake.

Sehemu moja ya uchunguzi huo inasema kuwa, kutokana na kueneza fikra za mrengo wenye misimamo mikali wa kulia baada ya Uingereza kujiondoa katika Umoja wa Ulaya, watu 4 kati ya kila Waingereza 10 wanaogopa kueleza itikadi na mitazamo yao kuhusiana na wahajiri na asilimia 28 wanaamini kinyume chake. 

Uingereza ndiyo nchi pekee duniani inayofanya ujasusi kuhusu itikadi za raia wake kwa kutumia sheria ya Counter-Terrorism and Security Act.

Uzoefu umeonyesha kuwa sheria hiyo inalenga zaidi kaumu za wachache na wafuasi dini za walio wachache hususan Waislamu. 

Mwenyekiti wa Kamisheni ya Haki za Binadamu ya Kiislamu nchini Uingereza Massoud Shajareh anasema Waislamu wengi hawaripoti uhalifu unaotokana na fikra za kupiga vita Uislamu nchini humo kwa sababu zinazojulikana. 

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni