?>

Hali ya hatari yatangazwa mkoani Kivu Kaskazini huko Kongo

Hali ya hatari yatangazwa mkoani Kivu Kaskazini huko Kongo

Hali ya hatari iliyotangazwa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imeibua mjadala nchini humo.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Hali hiyo ya hatari imetangazwa katika mkoa wa Kivu ya Kaskazini huko mashariki mwa Kongo baada ya kuripotiwa mauaji ya raia wapatao 2,500 katika mikoa miwili iliyozingirwa; na hivyo kuifanya idadi ya watu waliouliwa latika eneo hilo kuwa maradufu ikilinganishwa na ya mwaka mmoja uliopita. 

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Jean-Michel Sama Lukonde amesema kuwa, mzingiro na oparesheni zinazofanywa na jeshi huko Kivu Kaskazini zimesaidia kupunguza hujuma na vitendo viovu. Amesema serikali inafikiria kuainisha maeneo ambapo hatua za ulinzi zitadumishwa kwa kuzingatia kuwa mashambulizi na vitendo vya unyanyasaji vinatekelezwa katika maeneo maalumu. 

Jeshi la Congo DR limezidisha oparesheni zake dhidi ya ngome za makundi ya waasi chini ya uongozi wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Jean Michel Sama Lukonde. Kapteni Anthony Mualushayi Msemaji wa Jeshi katika mji wa Beni huko Kivu Kaskazini ameeleza kuwa, waasi wa ADF wamefurushwa katika ngome zao nyingi zilizokuwa zikitumiwa kutoa mafunzo na mashambulizi  dhidi ya maeneo ya jeshi na raia. 

Inafaa kuashiria hapa kuwa, mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka jana, jeshi la Uganda liliingia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa lengo la kushiriki latika oparesheni ya kuwasaka waasi wa kundi la ADF ambao ni tawi la kundi la kigaidi la Daesh katikati ya Afrika. Waasi hao wanatuhumiwa kufanya mauaji ya umati huko Kongo tangu muongo wa tisini na mashambulizi mengine ya karibuni huko Uganda. 

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*