?>

HAMAS: Adui Mzayuni amelenga kuuhujumu utambulisho wa Quds inayokaliwa kwa mabavu

HAMAS: Adui Mzayuni amelenga kuuhujumu utambulisho wa Quds inayokaliwa kwa mabavu

Msemaji wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS amelaani upanuzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni unaofanywa na utawala haramu wa Israel katika mji wa Baitul Muqaddas unaokaliwa kwa mabavu na kueleza kwamba, kwa hatua zake hizo, adui Mzayuni amelenga kuuhujumu utambulisho wa Kipalestina wa mji huo wa Quds unaokaliwa kwa mabavu.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Fawzi Barhum amesisitiza kuwa, ujenzi huo wa vitongoji unaofanywa na utawala wa Kizayuni utapelekea Wapalestina wengi zaidi wabaki bila makazi na kuwa wakimbizi, jambo ambalo linashuhudiwa hivi sasa katika eneo la Sheikh Jarrah, katika mji huo wa Baitul Muqaddas unaokaliwa kwa mabavu.

Msemaji wa Hamas amebainisha kuwa, hapana shaka yoyote kwamba, hatua za Wazayuni za kupanua ujenzi wa vitongoji katika mji wa Quds unaokaliwa kwa mabavu na hasa eneo la Sheikh Jarrah zimelenga kuhujumu utambulisho wa Kipalestina wa mji huo.

Barhum ameongeza kuwa, kuongezeka ujenzi wa vitongoji, hasa katika mji wa Sheikh Jarrah hakukubaliki; na kukabiliana na mipango hiyo ya kiuadui ya utawala wa Kizayuni ni jukumu la kitaifa.

Wakati huohuo harakati ya Hamas imewatolea mwito Wapalestina wote kukabiliana na mipango ya kiuadui ya utawala wa Kizayuni katika ardhi unazozikalia kwa mabavu na kusisitiza kuwa, Wapalestina wataweza hatimaye kuzima njama za viongozi wa utawala huo ghasibu.

Aidha imeiomba Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na Jamii ya Kimataifa zichukue hatua kukabiliana na mipango ya utawala wa Kizayuni huko Quds, ikiwemo ya kuwahamisha kwa nguvu Wapalestina na kuwanyang'anya nyumba na ardhi zao.

Desemba 23, 2016 Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio nambari 2334 lililoutaka utawala haramu wa Kizayuni wa Israel usimamishe kikamilifu shughuli zote za ujenzi wa vitongoji katika maeneo ya Palestina.../

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*