?>

HAMAS: Takwa la Wapalestina kwa Mamlaka ya Ndani ya Palestina ni kukata kikamilifu uhusiano na Marekani

HAMAS: Takwa la Wapalestina kwa Mamlaka ya Ndani ya Palestina ni kukata kikamilifu uhusiano na Marekani

Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) amesisitiza kuwa, takwa la taifa la Palestina kwa Mamlaka ya Ndani ya Palestina ni kukata kikamilifu uhusiano wake na serikali ya Marekani.

(ABNA24.com) Fawzi Barhoum amesema hayo katika mkutano wake na waandishi wa habari na kueleza kwamba, kuendelea kuwepo mikutano na mazungumzo ya mara kwa mara baina ya maafisa wa ngazi za juu wa usalama wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina na wenzao wa Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA) ni ishara ya wazi kwamba, Mamlaka ya Ndani ya Palestina na vyombo vyake vya kiintelijensia vingali vinaitegemea Washington.

Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS)  amesema kwamba, vikao hivyo vya pande mbili vinafanyika katika hali ambayo, nafasi na mchango wa serikali ya Marekani katika mpango wa Muamala wa Karne unaolenga kuyaangamiza malengo matukufu ya Palestina uko wazi na bayana kabisa.

Aidha afisa huyo wa ngazi za juu wa Hamas ameongeza kuwa, Mamlaka ya Ndani ya Palestina imeendelea kupuuza takwa la Wapalestina ambalo ni kukata kikamilifu mamlaka hiyo uhusiano wake na serikali ya Marekani.

Wakati huo huo, Nabil Abu Rudainah, msemaji wa serikali ya Mamlakak ya Ndani ya Palestina  alisema Jumapili iliyopita kwamba, ushirikiano wa kiusalama baina ya mamlaka hiyo na utawala haramu wa Israel ungali unaendelea na kwamba, haujasimamishwa.

.............
340


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni