?>

HAMAS: Tuko pamoja na Syria katika makabiliano yake na utawala haramu wa Israel

HAMAS: Tuko pamoja na Syria katika makabiliano yake na utawala haramu wa Israel

Mmoja wa viongozi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema kuwa, misimamo ya harakati hiyo katu haijabadilika na kwamba, inaendelea kuiunga mkono nchi ya Syria katika makabiliano yake na utawala haramu wa Israel.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Dakta Mahmoud al-Zahar, afisa wa ngazi za juu wa Hamas amesisitiza kuwa, harakati hiyo ya muqawama iko bega kwa bega na taifa la Syria katika makabiliano yake na utawala vamizi wa Israel.

Al-Zahar amesema hayo katika mahojiano yake na Kanali ya Televisheni ya al-Mayadin na kubainisha kwamba, hakuna mashinikizo ya aina yoyote ile ambayo yataweza kuilazimisha Hamas ibadilishe misimamo yake katika kukabiliana na utawala ghasibu wa israel.

Kadhalika kiongozi huyo wa ngazi za juu wa  Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema kuwa, kile ambacho ni cha lazima kwa sasa ni kuvuka salama kipindi hiki hususan baada ya mataifa mengi ya Kiarabu kubadilisha misimamo yao na kuweko hali kama hiyo pia katika uga wa kimataifa.

Dakta al-Zahar ameashiria pia kadhia ya ulazima wa kuweko umoja na mshikamano wa kitaifa Palestina na kusisitiza kuwa, nguuvu ya muqawama ipo katika umoja wa kitaifa na kwamba, umoja huu unasaidia mno katika kuboresha hali ya mambo katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, Quds na Ukanda wa Gaza.

Ameeleza pia udharura wa kufanyika mikutano mikubwa, na jumuishi baina ya makundi ya Palestina kwa ajili ya kutoa majibu ya maswali mengi yanayoulizwa kuhusiana na kuweko hitilafu na mivutano baina yao, ambapo moja ya masuala hayo ni kadhia ya uchaguzi.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni