?>

HAMAS yalaani jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya Kibla cha Kwanza cha Waislamu

HAMAS yalaani jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya Kibla cha Kwanza cha Waislamu

Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema kuwa, harakati hiyo kamwe haitoruhusu utawala wa Kizayuni uendelee kufanya jinai dhidi ya Msikiti wa al Aqsa (Kibla cha Kwanza cha Waislamu).

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Kituo cha Upashaji Habari cha Palestina kimemnukuu Ismail Hania akisema hayo katika tamko lake rasmi na kuionya Israel kwamba iache kutekeleza mipango yake ya kikhabithi kwa kutumia vibaya mgogoro wa corona na kuongeza kuwa, njama za namna hiyo za Wazayuni kamwe hazitofanikiwa.

Mkuu huyo wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amelaani pia jinai ya utawala wa Kizayuni ya kumuweka chini ya ulinzi Khatibu wa Msikiti wa al Aqsa, Sheikh  Ekrima Sa'id Sabri na kusema kuwa kitendo hicho ni kukanyaga na kuponda haki ya kuabudu na uhuru wa kuingia kwenye eneo hilo takatifu, bali ni sehemu ya njama za Tel Aviv za kutaka kuwafanya Waislamu wasiingie msikitini humo.

Ismail Hania aidha amewataka wakuu na viongozi wa nchi za Kiarabu na Kiislamu kutekeleza ipasavyo majukumu yao ya kidini na kihistoria kuhusu Kibla cha Kwanza cha Waislamu yaani Masjidul Aqswa.

Askari wa shirika la kijasusi la utawala wa Kizayuni MOSSAD jana Ijumaa waliivamia nyumba ya Sheikh Ekrima Sabri, Khatibu wa Msikiti wa al Aqsa katika mji mtakatifu wa Baytul Muqaddas unaokaliwa kwa mabavu na Wazayuni na kumteka nyara na kumpeleka kusikojulikana.
Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni