?>

HAMAS yatupilia mbali ombi la Marekani la kuweko uhusiano wa kidiplomasia baina yao

HAMAS yatupilia mbali ombi la Marekani la kuweko uhusiano wa kidiplomasia baina yao

Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu wa Palestina HAMAS ametupilia mbali ombi la Marekani la kutaka Washingto iwe na uhusiano wa kisiasa na harakati hiyo ya Kiislamu.

(ABNA24.com) Akizungumza na kanali ya televisheni ya Al-Mayadin ya nchini Lebanon, Ismail Haniyeh sambamba na kutupilia mbali kufanya uhusiano wowote wa kidiplomasia na Marekani, kwa mara nyingine amesisitizia kufungwa njia zote za udhibiti wa Washington kwa eneo hili.

Haniyeh amesema kuwa umoja wa Wapalestina kwa ajili ya kukabiliana na mpango wa Marekani wa Muamala wa Karne ni wenye umuhimu sana na kubainisha kuwa, juhudi za aina yoyote kwa ajili ya kuibua tofauti kati ya harakati ya Hamas na Jihadul-Islami, zimefeli kwa kuwa muqawama wa Ukanda wa Gaza haukubali kushindwa.

Akizungumzia safari yake ya hivi karibuni mjini Moscow, Russia Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu wa Palestina HAMAS amesema kuwa ili kuweza kufikia mtazamo mmoja, harakati hiyo iliwasilisha machaguo yake manne kwa Russia ambayo ni uchaguzi mkuu, kufanyika bunge la kitaifa la Palestina nje ya mji wa Ramallah, kufanyika kwa kongamano kuu la kitaifa la Palestina mjini Cairo Misri na kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa ya Palestina.

Jumatatu iliyopita Ismail Haniyeh akiwa mjini Moscow alikutana na Sergey Lavrov, Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia na kujadiliana naye mipango ya kisiasa ya ukombozi wa Palestina na njia za utatuzi wa kudumu na amani katika eneo la Asia Magharibi.

.............
340


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni