?>

Hamza Abdi Barre ateuliwa kuwa Waziri Mkuu wa Somalia

Hamza Abdi Barre ateuliwa kuwa Waziri Mkuu wa Somalia

Hamza Abdi Barre ameteuliwa kuwa waziri mkuu mpya wa Somalia huku jitihada zikiendelea za kuleta utulivu wa kudumu wa kisiasa na kiusalama katika nchi hiyo ya Pembe ya Afrika ambayo pia inakumbwa na baa la njaa.

Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)- ABNA - Rais mpya wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamud amemtua Abdi Barre Jumatano kuwa waziri mkuu wa nchi hiyo. Katika tangazo hilo amesema, “Nimezingatia uamuzi wangu baada ya kutathmini ufahamu, uzoefu, pamoja na uwezo wa Hamza, kisha nikafikia hitimisho kwamba yeye ndio mtu sahihi, ambaye anaweza kutekeleza jukumu hili jipya katika Somalia hii mpya kwa wakati huu mpya,” amesema.

Amewataka wabunge kumuidhinisha Waziri Mkuu mpya haraka na kusema amemtaka Barre kuendeleza vipaumbele muhimu vya serikali mpya ikiwa ni pamoja na usalama, kukabiliana na ukame, maridhiano, maendeleo ya jamii na kukabiliana na majanga ya hali ya hewa.

Mohamoud alishinda urais kwa mara ya pili mwezi Mei baada ya kushikilia nafasi haiyo kuanzia mwaka 2012 hadi 2017. Uchaguzi huo ulifanyika baada ya kuahirishwa mara kadhaa huku nchi hiyo ikikumbwa na ukame mbaya zaidi katika kipindi cha miaka 40 huku magaidi wa Al Shabaab wakiendeleza hujuma zao.

Uteuzi wa Abdi Barre unakuja baada ya kuzuka mvutano mkubwa baina ya rais wa zamani Mohammad Abdullahi Mohammad na waziri mkuu wake Hussein Roble. Mvutano wa wawili hao uliibua mgawanyiko pia katika vikosi vya usalama na hivyo kuvuruga vita dhidi ya magaidi wa Al Shabaab ambao bado wanadhibiti maeneo makubwa ya nchi hiyo.342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*