?>

Haniya: Njia mwandishi habari Mpalestina aliyeuawa shahidi itaendelea

Ismail Haniya, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) ameulaani vikali utawala wa Kizayuni wa Israel kwa kumuua shahidi Shireen Abu Akleh mwandishi habari Mpalestina wa Kanali Al Jazeera.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Katika taarifa, Haniya amesema Shireen Abu Akleh alitoa maisha yake muhanga katika njia ya kufichua jinai za kutisha zaidi za Wazayuni katika zama hizi.

Shireen Abu Akleh mwandishi habari Mpalestina aliuawa shahidi leo kwa kupigwa risasi na askari wa utawala wa Kizayuni wa Israel wakati akiakisi matukio na mapigano katika kambi ya wakimbizi ya Jenin.

Kufuatia jinai hiyo ya Wazayuni, Ismail Haniya amesema: " Shireen Abu Akleh atakumbukwa miongoni mwa kizazi ambacho kiliendeleza mapambano ya kuwatimua Wazayuni katika ardhi za Palestina."

Haniya ameongeza kuwa,  waandishi habari wa Palestina ni walinzi halisi na waendelezaji wa  njia aliyoichukua Shireen Abu Akleh na wengine kabla yake katika vyombo vya habari vya Palestina na hatimaye kuuawa shahidi."

Wakati huo huo Kamati ya Kuunga Mkono Waandishi Habari Wapalestina imetangaza kuwa, lengo la utawala wa Kizayuni wa Israel katika kuwalenga waandishi habari ni kuzuia kufichuliwa jinai za utawala huo dhidi ya watu madhulumu wa Palestina.

Kwingineko Lolwah Alkhater Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar amelaani kitendo cha utawala ghasibu wa Israel kumuua mwandishi huyo wa habari huku akitoa wito wa kuhitimishwa 'ugaidi wa kiserikali wa Israel.


342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*