?>

Hatua na jumbe za kindumakuwili za Marekani kuhusiana na JCPOA na Iran

Hatua na jumbe za kindumakuwili za Marekani kuhusiana na JCPOA na Iran

Moja ya zilizokuwa nara na madai muhimu ya Marekani wakati Rais Joe Biden alipoingia madarakani ni kuirejesha Washington katika makubaliano ya nyuklia yanayojulikana kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA).

Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)- ABNA - Pamoja na hayo na licha ya kupita takribani miaka miwili na nusu tangu kutolewa ahadi hizo, utendaji wa serikali ya Marekani wenye mgongano katika uga wa misimamo na hatua zake kuhusiana na JCPOA na Iran umedhihirika wazi na bayana.

Katika hatua ya karibuni kabisa ya Washington kuhusiana na Iran, hatua ambayo ni kinyume kabisa na nara za kuindolea vikwazo Iran na kurejea katika makubaliano ya nyuklia ni ile iliyochukuliwa Alkhamisi iliyopita na Wizara ya Hazina ya Marekani ambayo ilitangaza vikwazo dhidi ya sekta ya petrokemikali ya Iran, na vilevile dhidi ya kampuni za China, Imarati na India zinazotuhumiwa kufanikisha kuuzwa mafuta ya Iran nje ya nchi. Katika radiamali yake kwa uamuzi huo, Mehdi Safari, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayehusika na Diplomasia ya Uchumi amesisitiza kuwa, vikwazo hivyo vipya vya Marekani havitaizuia Jamhuri ya Kiislamu kuendelea na shughuli zake za kila siku.

Rais Joe Biden wa Marekani alisisitiza mara chungu nzima huko nyuma juu ya ulazima wa kurejea nchi yake katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na alikuwa akidai kwamba, hilo litafanyika katika kipindi cha muda mfupi kabisa.

Pamoja na hayo, baada ya kufanyika duru nane za mazungumzo marefu huko Vienna Austria baina ya Iran na kundi la 4+1 na kuweko Marekani lakini kwa njia isiyo ya moja kwa moja, na licha ya kuonekana matumaini mwanzoni kuhusiana na kufikiwa makubaliano katika uga wa kuiondolea vikwazo Iran ilivyowekewa na Marekani na kisha Iran kurejea katika ahadi ilizojifunga nazo kwa mujibu wa JCPOA, lakini hadi sasa kungali kuna shaka na hata kumeibuka hali ya kukatisha tamaa kuhusiana na kadhia hiyo.

Ukweli wa mambo ni kuwa, Marekani inafanya njama za kukwamisha mazungumzo ya Vienna na kivitendo kuutupa mpira katika uwanja wa Iran na hivyo kuionyesha Tehran kuwa, ndio msababishaji wa hali hii isiyoelewekka. Hii ni katika hali ambayo, Iran metangaza wazi na dhahir shahir tena siyo mara moja wala mara mbili kuhusu matakwa yake na filihali ni serikali ya Biden ndio ambayo haitaki au haiwezi kutoa majibu chanya kwa matakwa haya ya kimantiki ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Kimsingi serikali ya Biden imeamua kufuata mkondo ulele wa mtangulizi wake yaani Donald Trump wa kutumia wenzo wa mashinikizo ya kiwango cha juu zaidi dhidi ya Iran. Hatua ya serikali ya Biden ya kutoa matakwa ambayo yapo nje kabisa ya makubaliano ya JCPOA imethibitisha kwamba, haina azma na irada ya lazima kwa ajili ya kutoa majibu chanya kwa matakwa ya kimantiki na ya kisheria ya Iran.

Hali hii imezidishwa na ukweli kwamba, takribani wabunge wote wa chama cha Republican na Wademokrat wengi wameeleza upinzani wao kwa makubaliano yoyote na Iran. Hivi sasa upande wa Magharibi na hata madola ya Ulaya hayana mtazamo mzuri juu ya uwezekano wa kufikiwa makubaliano mapya.

Makubaliano ya Vienna nayo yaliyokuwa na lengo la kuindolea vikwazo Iran yamesita na kusimama kwa miezi kadhaa sasa. Tangu kuanza kwa mazunguumzo hayo, serikali ya Marekani badala ya kutoa mapendekezo ya kibunifu na hivyo kusukuma mbele gurudumu la mazungumzo hayo, mara kadhaa imefanya njama za kuzituhumu pande mbalimbali ikiwemo Iran na Russia kwamba, zimekuwa zikifanya njama za kupunguza kasi ya mazungumzo hayo na hata kutia vizingiti  vya kuyakwamisha. Licha ya serikali ya Biden kukiri juu ya kugonga mwamba sera za mashinikizo na vikwazo dhidi ya Iran, lakini ingali inafuata mkondo huo na kuitisha Tehran kwa hili na lile.

342/Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*