?>

Hizbullah: Kuweko tayari muda wote Muqawama kumeizuia Israel kuivamia Lebanon

Hizbullah: Kuweko tayari muda wote Muqawama kumeizuia Israel kuivamia Lebanon

Naibu Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema kuweko tayari muda wote muqawama ndiko kulikoufanya utawala haramu wa Kizayuni wa Israel ughairi kuanzisha uvamizi dhidi ya Lebanon.

Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)- ABNA - Sheikh Naim Qassem ameyasema hayo katika hotuba aliyotoa kwa mnasaba wa maadhimisho ya kutimia miaka 40 ya kuasisiwa Hizbullah na kubainisha kuwa, mikakati makini iliyoratibiwa na Hizbullah katika maeneo ya kijeshi na kujizatiti yenyewe kwa silaha kwa ajili ya kukabiliana na hujuma za kila upande kumemshangaza adui; na huo ni moja ya ubunifu wa uongozi wa kipekee wa Shahidi Imad Mughniya.

Sheikh Naim Qassem ameashiria harakati za kisiasa za Hizbullah na akaeleza kwamba, Hizbullah ilianzisha harakati za kisiasa za kuingia bungeni 1991 na kuweza kutoa mchango katika upangaji wa sheria sambamba na kutoa huduma katika maeneo iliyowakilisha; hata hivyo hadi mwaka 2005 haikuwahi kushiriki katika serikali yoyote.

Naibu Katibu Mkuu wa Hizbullah amebainisha kuwa njama na ugaidi wa Marekani dhidi ya Lebanon sio pekee unaosababisha mgogoro na hali mbaya ya kiuchumi na kijamii, kwa sababu mgogoro huo unajumuisha pia ufisadi mkubwa uliosambaa serikalini katika ngazi zote; na mfumo wa kimatapo na kimadhehebu ndio unaowalinda mafisadi.

Sheikh Naim Qassem ameendelea kueleza kuwa, katika muda wa miaka 40 mhimili wa muqawama umepiga hatua mbele kwa kupata ushindi mkubwa, kuleta mageuzi ya kimsingi katika eneo, kushinda njama za pamoja za Marekani na Israel, kuleta mwamko kwa wananchi wa Palestina, kuihuisha kadhia ya Palestina na Quds na kuifanya kuwa kipaumbele cha dira katika njia ya ukombozi na kujitawala.

Hizbullah iliasisiwa mwaka 1982. Katika muda wote huu wa miongo minne, harakati hiyo ya mapambano na muqawama imepata nguvu zaidi na kuweza kujipatia ushindi mkubwa wa kijeshi mara mbili katika mwaka 2000 na 2006 dhidi ya Israel na kuthibitisha kuwa mlinzi wa kudhamini maslahi ya taifa ya Lebanon.../

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*