?>

Hizbullah yalaani shambulio la kigaidi dhidi ya jeshi la Misri

Hizbullah yalaani shambulio la kigaidi dhidi ya jeshi la Misri

Harakati ya Hizbullah ya Lebanon imelaani shambulio la kigaidi lililolenga askari wa jeshi la Misri katika jangwa la Sinai.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Japokuwa mashambulio kadhaa ya anga na nchi kavu yaliyofanywa na jeshi la Misri katika miaka ya karibuni yamepunguza nguvu za kundi la kigaidi la "Wilayat ya Sinai", lakini mashambulio ya kigaidi dhidi ya askari wa jeshi la Misri yangali yanaendelea.

Jeshi la Misri jana Jumamosi lilitangaza kuwa wanajeshi wake 10 na afisa wake mmoja wameuawa katika shambulio la kigaidi lililolenga mtambo wa kuchujia maji mashariki ya Mfereji wa Suez.

Kwa mujibu wa taarifa ya jeshi la Misri, askari wengine watano wa jeshi hilo wamejeruhiwa katika operesheni ya kuwasaka na kuwaandama magaidi wa kundi hilo.

Shirika la habari la al- A'hd limeripoti kuwa, harakati ya Hizbullah ya Lebanon imeeleza katika taarifa iliyotoa leo kwamba, lengo la hatua hiyo iliyochukuliwa na magenge ya kigaidi ni kuvuruga amani na uthabiti wa Misri, kuzibabaisha fikra za waliowengi kuhusiana na ugaidi wa Kizayuni katika Palestina inayokaliwa kwa mabavu na kulitumbukiza tena eneo kwenye mzunguko usio na mwisho wa fitna na mapigano.

Katika taarifa yake hiyo, Hizbullah imerudia tena kubainisha msimamo wake wa hapo kabla kuhusu udharura wa maulamaa wa kiislamu kukabiliana na fikra haribifu za ukufurishaji na kuchukuliwa hatua za kuzuia fikra hizo katika Ulimwengu wa Kiislamu kupitia njia za kiuelimishaji na kisiasa.

Kutokana na muundo wa idadi ya watu na mfumo wa kikabila wa watu wake; na vilevile kwa kuzingatia mazingira ya kijiografia ya mabonde na miinuko iliyoko kwenye Peninsula ya Sinai, tangu mwaka 2011 na kuendelea, magaidi wameanzisha harakati zao katika eneo hilo; na baada ya kuibuka kundi la kigaidi na ukufurishaji la DAESH (ISIS), magaidi hao wametangaza kiapo cha utiifu kwa kundi hilo na kulipa genge lao jina la "Wilayat ya Sinai".../

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*