?>

Hizbullah: Yeyote mwenye kuwa pamoja na Iran na muqawama atapata ushindi

Hizbullah: Yeyote mwenye kuwa pamoja na Iran na muqawama atapata ushindi

Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, tajiriba inaonesha kuwa, yeyote mwenye kuwa pamoja na Iran au muqawama basi ataibuka na ushindi.

(ABNA24.com) Sheikh Naim Qassim amesema hayo katika hotuba yake kwa mnasaba wa maadhimishisho ya miaka 41 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu na kueleza kuwa, matatizo ya Asia Magharibi chimbuko lake ni uwepo wa utawala haramu wa Israel na kukosoa vikali hatua ya Israel ya kuzikalia kwa mabavu ardhi za Palestina.

Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesisitiza kuwa, njia pekee ya wokozi kwa Wapalestina ni muqawama na mapambano ya silaha.

Sheikh Naim Qassim  amesema pia kuwa, ubeberu wa dunia haufahamu lugha nyingine isipokuwa mapambano kwa ajili ya kuikomboa Palestina na katu haiwezekani kuwategemea mabeberu wa dunia au Marekani katika kuitatua kwa njia za kisiasa migogoro ya eneo la Asia Magharibi.

Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesema bayana kwamba, ni taifa shupavu, shujaa na lenye kuendesha mapambano la Palestina ambalo limeusambaratisha mpango wa Marekani wa Muamala wa Karne hata kabla ya kutekelezwa kwake.

Sheik Naim Qassim amehoji kwa kusema kuwa, kwa nini tunataka kupambana na Muamala wa karne uliokufa kabla ya kuzaliwa? Ni kwa sababu hatutaki ibakie chembe ya dhana katika fikra za walimwengu kwamba, mipango inayohusiana na Palestina inaweza kutekelezwa bila ya ridhaa na matakwa ya Wapalestina wenyewe.

............
340

(ABNA24.com)

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni