?>

Human Right Watch: Mzingiro dhidi ya Ukanda wa Gaza ni jinai dhidi ya binadamu

Human Right Watch: Mzingiro dhidi ya Ukanda wa Gaza ni jinai dhidi ya binadamu

Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch limetangaza kuwa, mzingiro dhidi ya Ukanda wa Gaza huko Palestina unaofanywa na utawala wa Kizayuni wa israel ni jinai dhidi ya binadamu.

Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)- ABNA - Taarifa ya Human Rights Watch iliyotolewa kwa mnasaba wa miaka 15 ya kuzingirwa eneo la Ukanda wa Gaza imesisitiza kuwa, mzingiro dhidi ya eneo hilo ni jinai dhidi ya binadamu na ni hatua ya kibaguzi na kidhulma dhidi ya watu milioni moja wanaoishi katika eneo hilo.

Sehemu nyiingine ya taarifa ya Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch imeeleza kuwa, mzingiro dhidi ya Ukanda wa Gaza umesambaratisha kikamilifu uchumi wa eneo hilo na watu wengi katika eneo hilo wamenyimwa fursa ya kujipatia maendeleo.

Umoja wa Mataifa nao umewahi kusisitiza mara nyingi katika ripoti zake kwamba, mzingiro wa utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza unakiuka sheria za kimataifa.

Umoja wa Mataifa na baraza lake la usalama zinakosolewa kwa kutochukua hatua yoyote dhidi ya utawala ghasibu wa Israel unaotekkeleza mzingiro dhiidi ya Ukanda wa Gaza.

Utawala wa Kizayuni wa Israel unalizingira eneo la Ukanda wa Gaza tangu mwaka 2006 wakati Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) ilipoibuka na ushindi katika uchaguzi wa Bunge la Palestina.

Tangu wakati huo Israel imekuwa ikizuia kuingizwa bidhaa zote muhimu katika eneo hilo kama vile chakula, dawa, vifaa vya ujenzi na kadhalika na kulifanya eneo hilo kukabiliwa na hali mbaya. 


342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*