?>

Ibada ya usiku wa Lailatul Raghaib katika Msikiti wa Hagia Sophia, Uturuki

Ibada ya usiku wa Lailatul Raghaib katika Msikiti wa Hagia Sophia, Uturuki

Ibada ya usiku wa Lailatul Raghaib imefanyika katika msikiti wa kihistoria wa Hagia Sophia mjini Istanbul, Uturuki.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Usiku wa Lailatul Raghaib ni usiku wa kuamkia Ijumaa ya kwanza ya Mwezi wa Rajab na umetajwa kuwa miongoni mwa nyakati bora zaidi ambazo Mwenyezi Mungu SWT hujibu Dua za waja Wake. Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, jana waumini walimiminika katika msikiti huo kwa ajili ya Sala na Dua maalumu katika usiku huo. Waumini walioshiriki katika ibada ya usiku wa Lailatul Raghaib walizingatia kanuni za kiafua za kuzuia kuenea ugonjwa wa Corona. Jengo hilo Hagia Sophia lilijengwa mwaka 537 Miladia (CE) na lilipata umaarufu kutokana na kuba lake adhimu na wakati huo lilikuwa jengo kubwa zaidi duniani. Tokea mwaka 537 hadi 1453 lilikuwa ni Kanisa la Mashariki la Kiothodoxi na makao makuu ya Kasisi Mkuu wa Constantinople. Kwa muda mfupi, kati yaani kati ya mwaka 1204 hadi 1261, jengo hilo liligeuzwa na Wapiganaji wa Nne wa Msalaba kuwa Kanisa Katoliki. Wakati watawala wa silsila ya Wauthmaniya (Ottomans) walipouteka mji huo, mnamo mwaka 1453 Fatih Sultan Mehmet aliagiza jengo la Hagia Sophia litumike kama msikiti. Hadhi hiyo ya Hagia Sophia kama msikiti iliendelea kwa muda wa miaka 482 hadi mwaka 1935 wakati muasisi wa Jamhuri ya Uturuki, Mustafa Kemal Ataturk alipoagiza ligeuzwe na kuwa jengo la makumbusho. Mwaka jana Uturiki ilitangaza kuwa Hagia Sophia imerejea katika hadhi yake ya Msikiti. Swala ya kwanza ya Ijumaa iliswaliwa katika Msikiti wa Hagia Sophia, Istanbul Uturuki baada ya zaidi ya miaka 86 ambapo maelfu ya waumini wameshiriki katika swala hiyo mnamo Julai 24, 2020.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni