?>

Ibrahim Raeisi: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itaendelea kuitetea Palestina

Ibrahim Raeisi: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itaendelea kuitetea Palestina

Sayyid Ibrahim Raeisi, Rais mteule wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Tehran itaendelea kuiunga mkono na kuitetea nchi ya Palestina.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Rais mteule wa Iran amesema hayo katika mazungumzo yake kwa njia ya simu na Ismail Hania Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS na Ziad Nakhalah, Katibu Mkuu wa Harakati ya Jihadul Islami ya Palestina.

Ayatullah Raeisi kwa mara nyingine tena ametoa mkono wa pongezi kufuatia ushindi mkubwa wa taifa la Palestina katika Vita vya Seif al-Quds dhidi ya utawala haramu wa Israel.

Rais mteule wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amewahakikishia viongozi hao kwamba, Iran itaendelea kuliunga mkono na kulitetea taifa madhulumu la Palestina.

Ameongeza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itaendeleza himaya na uungaji mkono wake kwa Palestina hadi Quds Tukufu itakapokombolewa.

Kwa upande wake, Ismail Hania, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS sambamba na kumpongeza Ibrahim Raesi kwa kuibuka na ushindi katika uchaguzi wa Rais wa mwezi uliopita wa Juni ameishukuru na kuipongeza Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa himaya na uungaji mkono wake kwa kadhia ya Palestina.

Naye Ziad Nakhalah, Katibu Mkuu wa Harakati ya Jihadul Islami ya Palestina amemtakia mafanikio mema Ibrahim Raesi katika majukumu yake mapya ya urais na amesifu uungaji mkono wa Iran kwa taifa la Palestina na harakati ya muqawama.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*