?>

IDEA: Kwa mara ya kwanza, Marekani imeingia kwenye orodha ya nchi zenye mmomonyoko wa demokrasia

IDEA: Kwa mara ya kwanza, Marekani imeingia kwenye orodha ya nchi zenye mmomonyoko wa demokrasia

Taasisi ya Kimataifa kwa ajili ya Demokrasia na Usaidizi wa Uchaguzi, IDEA imesema, kwa mara ya kwanza Marekani imeingia kwenye orodha ya nchi duniani zinazokabiliwa na mmomnyoko wa demokrasia.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: IDEA imeeleza katika ripoti yake ya kila baada ya miaka miwili ambayo imetolewa kwa anuani ya "Hali ya Demokrasia Duniani Katika Mwaka 2021" kwamba, kwa mara ya kwanza, Marekani imeingia kwenye orodha ya nchi zinazokabiliwa na mmomnyoko wa kushuka kwa demokrasia.

Kwa mujibu wa asasi hiyo yenye makao yake mjini Stockholm, Sweden, mwaka 2019, ndipo ulipoanza mwenendo wa kurudi nyuma na kuporomoka demokrasia nchini Marekani.

Kwa mujibu wa Taasisi ya Kimataifa ya kwa ajili ya Demokrasia na Usaidizi wa Uchaguzi, kuvurugika demokrasia nchini Marekani kunashuhudiwa katika ongezeko la changamoto zinazohusiana na matokeo ya uchaguzi, hatua za kukandamiza ushiriki wa watu katika uchaguzi pamoja mpasuko wa kambi mbili katika jamii ya nchi hiyo, ambao ni moja ya mabadiliko yenye kutia wasiwasi mkubwa zaidi.

Ripoti hiyo ya IDEA imeongeza kuwa, idadi ya nchi ambazo zimekumbwa na mmomonyoko na kupungua kwa demokrasia katika kipindi cha muongo mmoja uliopita imeongezeka maradufu na kujumuisha robo moja ya idadi ya watu wote duniani.

Mbali na Marekani, Brazil na India zimetajwa pia kuingia kwenye orodha ya nchi zilizokumbwa na mmomonyoko wa demokrasia, ambapo kwa upande wa nchi za Ulaya inazijumuisha Hungary, Poland, Serbia na Slovenia.

Kwa mtazamo wa mabara, ripoti ya IDEA imesema Afrika ndiyo iliyoathirika zaidi. 

Seema Shah, ambaye ni miongoni mwa waandishi wa ripoti hiyo amesema, "kulikuwa na maendeleo ya ajabu mwanzoni mwa miaka ya 1990 ambayo yalimpa kila mtu matumaini makubwa, lakini idadi ya mifumo ya demokrasia barani Afrika imepungua kutoka 22 mwaka 2015 hadi 18 mwaka 2020," 

Ripoti ya Taasisi ya Kimataifa ya kwa ajili ya Demokrasia na Usaidizi wa Uchaguzi imeongeza kuwa kwa sasa, asilimia 70 ya watu duniani wanaishi katika nchi zenye tawala zisizo za kidemokrasia au zinazorudi nyuma katika demokrasia.../

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*