?>

Iran: Hatutoruhusu kufanikiwa njama za Wazayuni za kueneza chuki dhidi yetu

Iran: Hatutoruhusu kufanikiwa njama za Wazayuni za kueneza chuki dhidi yetu

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran katika masuala ya kisiasa amesema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu haitoruhusu kufanikiwa njama za Wazayuni za kueneza chuki chidi ya Tehran.

Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)- ABNA - Ali Bagheri Kani amesema hayo katika Chuo Kikuu cha Tehran na kuongeza kuwa, maadui wa taifa la Iran waelewe kuwa, taifa hili ambalo limefanikiwa kushinda vita vya vikwazo vya kiwango cha juu zaidi vya Marekani na kuwalazimisha viongozi wa White House kutangaza kushindwa vikwazo vyao hivyo, kamwe halitoruhusu kufanikiwa njama za Wazayuni za kueneza chuki dhidi yake.

Tangu ilipoingia madarakani serikali ya 13 ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hapo tarehe 3 Agosti 2021, imetangaza kuwa siasa zake ni kuweka mlingano katika siasa za nje za Jamhuri ya Kiislamu pamoja na kulipa kipaumbele suala la kustawisha ushirikiano na nchi jirani na za ukanda huu mzima.

Siasa hizo ni za kuelekea zaidi upande wa mashariki mwa dunia na kushirikiana zaidi na taasisi za kieneo na za kimataifa kama Mkataba wa Shanghai na Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya ECO.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran katika masuala ya kisiasa ameongeza kuwa, siasa za serikali ya hivi sasa ya Iran ni kuhakikisha vitisho vinapungua, fursa zinatumiwa vizuri na chombo cha diplomasia kinakuwa amilifu zaidi katika mabadiliko makubwa ya haraka na ya kila namna ya kieneo na kimataifa.

Amesema, Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran inatambua kwamba ni jukumu lake kuleta imani thabiti ya kitaifa kuhusu maudhui kuu za siasa za nje za Jamhuri ya Kiislamu.


342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*