?>

Iran imefanyia majaribio chombo cha kurusha sataliti kinachotumia fueli mango

Iran imefanyia majaribio chombo cha kurusha sataliti kinachotumia fueli mango

Kamanda wa Kikosi cha Anga cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema Iran imefanyia majaribio yaliyofana injini ya kwanza ya Iran yenye kubeba satalaiti katika anga za mbali ambayo inatumia fueli mango.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Akizungumza Alhamisi mjini Qum, Kamanda wa Kikosi cha Anga cha IRGC Jenerali Amir-Ali Hajizadeh amesema: "Katika majaribio hayo yaliyofana, injini yenye uzito wa tani 66 yenye kutumia fueli mango imetumika."

Jenerali Hajizadhe amesema katika sekta ya anga za mbali, kuna nukta mbili muhimu nazo ni satalaiti na chombo cha kubeba sataliti. Ameongeza kuwa, "Katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, vyombo vya Iran vya kubeba satalaiti vimekuwa vikifanyia majaribio utumizi wa fueli mango na kuanzia sasa Iran itakuwa ikituma idadi kubwa ya satalaiti katika anga za mbali kwa kutumia injini zisizo gharimu kiasi kikubwa cha fedha."

Kamanda wa Kikosi cha Anga cha IRGC ameendelea kubaini kuwa: "Satalaiti mpya za Iran zimeundwa kwa kutotumia chuma na teknolojia hii inatumiwa na nchi nne tu duniani."

Jenerali Hajizadeh ameendelea kusema kuwa hivi sasa Iran imepiga hatua kubwa katika sekta ya anga za mbali na uundaji satalaiti kiasi kwamba hata adui akiua wanasayansi au akitoa vitisho na kuweka vikwazo hawezi kuangamiza sekta hiyo.

Aidha amesema Kamandi Kuu ya Jeshi la Marekani, CENTCOM, imekiri kuwa Iran sasa imepata uwezo mkubwa katika uga wa utengenezaji wa ndege zisizo na rubani au drone.

Kamanda huyo wa ngazi za juu wa IRGC aidha amesema Baraza la Atlantiki limekiri kuwa mwaka 2020 meli za kivita za Marekani zilizo katika eneo la Ghuba ya Uajemi hazikuweza kuzuia Iran kufanya majaribio ya makombora yake ya kujihami. Aidha meli hizo za kivita za Marekani hazikuweza kuzuia hujuma ya Jeshi la Iran dhidi ya kituo cha kijeshi cha Marekani cha Ain al Assad nchini Iraq.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*