?>

Iran imeuza bidhaa zake za nano katika zaidi ya nchi 45

Iran imeuza bidhaa zake za nano katika zaidi ya nchi 45

Katibu wa Idara ya Taifa ya Ustawi wa Teknolojia ya Nano nchini Iran amesema hivi sasa bidhaa za teknolojia hiyo zilizotengenezwa Iran zinauzwa katika zaidi ya nchi 45 duniani.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Saeed Sarkar Katibu wa Idara ya Kitaifa ya Ustawi wa Teknolojia ya Nano nchini Iran  amesema bidhaa za Iran za teknolojia ya nano zimeuzwa katika nchi kama Australia, Korea Kusini, China, bara Ulaya na Amerika ya Latini.

Amesema teknolojia mpya kama teknolojia ya nano ni muhimu sana duniani, na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeweza kupata nafasi muhimu katika teknolojia hiyo.

Sarkar amesema Iran imenufaika na teknolojia ya nano katika sekta 18 za viwanda na hivi karibuni pia bidhaa mpya zitazalishwa katika uga huo.

Amesema kwa mafanikio ambayo Iran imepata, si tu kuwa itaweza kukidhi mahitaji yake bali pia itakidhi mahitaji ya nchi zingine duniani.

Miaka 42 baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, kati ya mafanikio makubwa ambayo yameweza kupatikana ni ustawi wa kasi katika uga wa sayansi na teknolojia.

Iran inahesabiwa kuwa miongoni mwa nchi 10 bora duniani katika uga wa teknolojia ya nano.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*