?>

Iran inabeba mzigo mkubwa zaidi wa wakimbizi katika eneo

Iran inabeba mzigo mkubwa zaidi wa wakimbizi katika eneo

Mwakilishi maalumu wa Jamhuri ya Kiislamu y Iran katika masuala ya Afghanistan amesema: "Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, kutokana na vigezo vyake vya Kiislamu na kibinaadamu imekubali kubeba mzigo mkubwa zaidi wa wakimbizi katika eneo.

Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)- ABNA - Leo tarehe 20 Januari ni Siku ya Kimataifa ya Wakimbizi. Hii ni siku ya kuwaenzi mamilioni ya wanadamu  wakiwemo mamilioni ya raia wa Afghanistan ambao kutokana na mateso na masaibu na wamelazimika kuwa wakimbizi kufuatia miongo kadhaa ya vita katika nchi yao pamoja na umasikini ambao umetokana na nchi yao kukaliwa kwa mabavu na wavamizi wa kigeni. Hakuna shaka kuwa sababu kuu ambayo imepelekea Waafghani kukimbia ni nchi yao kuvamiwa na kukaliwa kwa mabavu na Marekani pamoja na waitifaki wake Wamagharibi.

Kwa miongo minne sasa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekuwa mwenyeji wa moja kati ya idadi kubwa zaidi ya wakimbizi duniani hasa raia wa Afghanistan. Hata katika kipindi cha vita vya kulazimishwa vya Iraq dhidi ya Iran na pia paoja na kuwepo vikwazo vya kidhalimu vya miongoni minne, Iran imeendelea kutoa huduma kwa mamilioni ya wakimbizi Waafghani ambao wanafanya kazi, kusoma na kuishi nchini bila vizingiti.

Akizungumza Jumanne, Hassan Kadhimi Qumo, Mwakilishi Maalumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika masuala ya Afghanistan ametuma ujumbe katika ukurasa wake wa Twitter kwa mnasaba wa Siku ya Kimataifa ya Wakimbizi na kuandika kuwa: "Hadaa ya wanaodai kutetea haki za binadamu na kuwapa himaya imebainika wakati wa kuwapokea wakimbizi Waafghani, Wasyria na Wairaqi kwani kinyume na wanavyodai wameonekana kuwa ni wabaguzi kutokana na namna wanavyowafadhilisha na kuwapendelea wakimbizi wa Ukraine."

Kadhimi Qumi amesema bila kupokea misaada ya mashirika ya kimataifa yanayodai kutetea wakimbizi, wakati wa mgogoro wa hivi karibuni nchini Afghanistan, Iran imepokea malaki ya wakimbizi wapya Waafghani na inawapa huduma wanazohitaji.

Baada ya kuja madarakani utawala wa Taliban nchini Afghanistan, idadi kubwa ya Waafghani walikimbia nchi yao kuelekea Iran. Pamoja na kuwepo  matatizo ya kiuchumi yatokanayo na vikwazo vya kidhalimu na pasina kuwepo misaada ya kimataifa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imewapokea kwa mikono miwili wakimbizi kutoka Afghanistan.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*