?>

Iran: Madai mapya ya wabunge wa Marekani yanalenga kuathiri mazungumzo ya JCPOA

Iran: Madai mapya ya wabunge wa Marekani yanalenga kuathiri mazungumzo ya JCPOA

Mjumbe mmoja wa Kamati ya Usalama wa Taifa na Siasa za Kigeni ya Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) amesema kuwa, msimamo mpya wa wabunge 220 wa Marekani kuhusu haki za binadamu nchini Iran unalenga kutoa taathira hasi kwa mazungumzo ya JCPOA.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Mahmoud Abbaszadeh Meshkini aidha amekosoa vikali msimamo wa wabunge 220 wa Marekani kuhusu haki za binadamu nchini Iran na kuongeza kuwa: Sasa hivi Marekani inateseka kwa matatizo ya kisiasa na kijamii, kila leo kunaripotiwa mauaji, ukatili na ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu huko Marekani, hivyo inashangaza kuona nchi hiyo inajipa uthubutu wa kuzungumzia haki za binadamu na kuchukua msimamo wa haki hizo kuhusu nchi nyingine.

Vile vile amesema, hakuna mshikamano wa kisiasa ndani ya Marekani na kusisitiza kwamba, wanachopaswa kufanya wabunge wa nchi hiyo ni kutatua matatizo yasiyo na idadi ya ndani ya nchi yao kwani wananchi wa nchi hiyo hivi sasa wanateseka kwa mambo yasiyo na kifani.

Mjumbe huyo wa Kamati ya Usalama wa Taifa na Siasa za Kigeni ya Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) vile vile amesema, wabunge wa Marekani wanafanya njama za kutumia hila mbalimbali kama madai ya uongo ya kuwapenda wananchi wa Iran, kulaani eti uvunjaji wa haki za binadamu Iran na kuingilia masuala yasiyowahusu ya mataifa mengine ili kuficha matatizo mengi ya ndani ya Marekani. Kila mtu anatambua vita vikubwa vya kiuchumi, kimatibabu na vya kidhalimu vilivyoanzishwa na Marekani dhidi ya taifa la Iran.

Itakumbukwa kuwa, zaidi ya wabunge 220 wa Marekani wametoa azimio liitwalo HR na kuituhumu Iran kwa kile walichodai ni kuvunja haki za binadamu na eti kuendesha ugaidi wa kiserikali.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*