?>

Iran: Marekani acheni vitisho, hamna nafasi Asia Magharibi

Iran: Marekani acheni vitisho, hamna nafasi Asia Magharibi

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH amesema kuwa, Wamarekani sasa wameelewa kuwa, kama wataendelea kung'ang'ania kubakia katika eneo la Asia Magharibi, basi wajiandae pia kupata hasara kubwa zaidi.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Meja Jeneral Hossein Salami amesema hayo katika mahojiano aliyofanyiwa na televisheni ya al Mayadin na huku akijibu vitisho vipya vya Washington dhidi ya Tehran kuhusu uwezekano wa kujibiwa ulipizaji kisasi wa mauaji ya kigaidi ya Luteni Jenerali Qasem Soleimani amesema, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni taifa huru na halifanyi mambo yake kwa amri ya Marekani.

Amesema, Asia Magharibi si eneo la Marekani; Wamarekani wanapaswa kuwa katika ardhi ya Marekani na si katika nchi za Iraq, Afghanistan, Bahrain, Syria na Kuwait.

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH  vile vile amesisitiza kuwa, Waislamu hawatoruhusu ardhi zao zikaliwe kwa mabavu na Wamarekani.

Mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka jana 2021 pia, Kamanda Mkuu huyo wa Jeshi la Iran la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH alisema kuwa, nguvu za Marekani zimedhoofika.

Alisema hayo katika sherehe za kumbukumbu  ya kuasisiswa jeshi la kujitolea (Basiji) la wanafunzi na kuongeza kuwa, katika siku za mwanzoni mwa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Marekani ilianzisha njama kubwa za kuyaangusha mapinduzi hayo lakini iliwabinikia kuwa Iran ni kitovu cha moyo wa dunia.

Kamanda Mkuu huyo wa SEPAH alisema pia kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imapata mafanikio makubwa huku ikiwa na uhuru wa kisiasa na uhuru wa kujiamulia masuala ya kiistratijia jambo ambalo limeipa fursa ya kujiainishia mustakabali wake na haisubiri amri kutoka kwa dola lolote ajinabi.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*