?>

Iran: Marekani haina azma ya kufunga jela ya Guantanamo

Iran: Marekani haina azma ya kufunga jela ya Guantanamo

Mkuu wa Masuala ya Kimataifa wa Idara ya Mahakama ya Iran ameukosoa vikali utawala wa Rais Joe Biden wa Marekani kwa kufeli kutekeleza ahadi yake ya kufunga jela ya kutisha ya Guantanamo Bay iliyoko nchini Cuba.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Kazem Gharib Abadi, ambaye pia ni Katibu wa Baraza Kuu la Haki za Binadamu la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alisema hayo jana Alkhamisi katika ujumbe aliotuma kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter, kwa mnasaba wa kuwadia mwaka wa ishirini tangu kuanzishwa jela hiyo ya kutisha ya Guantanamo.

Amesema si tu Marekani imekataa kutekeleza ahadi iliyotoa yenyewe ya kulifunga gereza hilo ambalo linawashikilia washukiwa kinyume cha sheria, lakini ina mpango wa kuipanua jela hiyo mwaka huu.

Afisa huyo mwandamizi wa kutetea haki za binadamu wa Iran amekumbusha kuwa, tangu jela ya Guantanamo ilipoanzishwa Januari 12, 2002, takriban watu 780 wameshikiliwa katika jela hiyo na hadi sasa tuhuma za kutenda uhalifu walizobambikiwa bado hazijathibitika. Gharib Abadi amesema wafungwa 39 wangali wanashikiliwa katika jela hiyo, iliyoko mashariki mwa Cuba katika eneo linalokaliwa kwa mabavu na Marekani.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*