?>

Iran na Hamas zataka nchi za Kiislamu kuchukua msimamo mmoja kukabiliana na Muamala wa Karne

Iran na Hamas zataka nchi za Kiislamu kuchukua msimamo mmoja kukabiliana na Muamala wa Karne

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) zimetoa wito kwa nchi za Kiislamu kuchukua msimamo mmoja kwa ajili ya kukabilina na mpango wa kibaguzi wa Marekani wa Muamala wa Karne.

(ABNA24.com) Wito huo umetolewa na Kazem Jalali, balozi wa Iran nchini Russia na Ismail Hania, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina katika mazungumzo yao mjini Moscow ambapo wamesisitiza kuwa, kuna udharura kwa nchi za Kiislamu kuwa na msimamo mmoja katika kukabiliana na mpango wa Marekani wa Muamala wa Karne.

Wawili hao wamejadili na kuzungumzia pia matuko ya kisiasa ya hivi karibuni huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu hasa baada ya kuzinduliwa mpango wa Muamala wa Karne.

Kadhalika balozi wa Iran mjini Moscow na Ismail Hania Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Hamas wamesisitizia  udharura wa kuendelezwa muqawama na mapambano kama njia pekee ya kukabiliana na utawala ghasibu wa Israel na kupatikana haki za Wapalestina.

Ismail Hania ameishuruku Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa himaya na uungaji mkono wake kwa kadhia ya Palestina na akamtaka balozi Jalali kumfikisha salamu zake na za wananchi wa Palestina kwa Ayatullah Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.

Ismail Hania, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS yupo ziarani nchini Russia akiuongoza ujumbe wa ngazi za juu wa harakati hiyo ikiwa ni kuitikia mwaliko wa viongozi wa Moscow.

...........
340


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni