?>

Iran: Tuko tayari kushirikiana na Iraq katika kukabiliana na harakati za kigaidi

Iran: Tuko tayari kushirikiana na Iraq katika kukabiliana na harakati za kigaidi

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amesema kuwa, Tehran iko tayari kushirikiana na Iraq katika kukabiliana na hakati za kigaidi nchini humo.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Saeed Khateebzadeh amelaani vikali hujuma ya kigaidi iliyofanyika katika kitongoji cha Sadr mjini Baghdad na kusema Iran iko tayari kushirikiana na serikali ya Iraq kupambana na harakati za kigaidi nchini humo. 

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran ameongeza kuwa, shambulizi hilo la kinyama linakariri uovu wa makundi ya kigaidi nchini Iraq na kwamba limewatia simanzi Waislamu waliokuwa wakijitayarisha kwa ajili ya sikukuu ya Idul Adh'ha. Khateebzadeh ametoa salamu za rambirambi za serikali na watu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa taifa na serikali ya Iraq na kuwaombea rehma na maghufira ya Mwenyezi Mungu walioaga dunia katika hujuma hiyo ya kigaidi. Vilevile amewatakia shifaa ya haraka majeruhi wa shambulizi hilo.

Watu wasiopungua 35 wameuawa na wengine zaidi ya 60 kujeruwa katika hujuma hiyo iliyotokelezwa na gaidi aliyekuwa amejifunga mabomu.

Kundi la kigaidi la Daesh limetangaza kuwa mwanachama wake anajulikana kwa jina la Abu Hamza alijilipua kwa mabomu katika mjumuiko wa Waislamu wa madhehebu ya Shia katika kitongoji cha Sadr mjini Baghdad na kuua makumi ya watu.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*