?>

Iran: Tumechelewa kulipa ada yetu UN kutokana na vikwazo vya kidhulma vya Marekani

Iran: Tumechelewa kulipa ada yetu UN kutokana na vikwazo vya kidhulma vya Marekani

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuhusu kusimamishwa haki ya kupiga kura Iran katika Umoja wa Mataifa kwamba anasikitika kusema kuwa, kwa mwaka wa pili mfululizo Tehran imeshindwa kulipa ada yake ya uanachama kwa Umoja wa Mataifa kutokana na vikwazo vya kidhulma na haramu vilivyowekwa na Marekani dhidi yake.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Shirika la habari la Iran Press limenukuu Saeed Khatibzadeh akisema hayo usiku wa kuamkia leo Alkhamisi na kuongeza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni mwanachama mkuu, mwanzilishi na amilifu wa Umoja wa Mataifa na miaka yote imekuwa ikilipa kikamilifu ada ya uanachama wake si kwa Umoja wa Mataifa tu lakini pia kwa mashirika na taasisi nyinginezo zote za kimataifa.

Pamoja na hayo amesema, vikwazo vya kidhulma vilivyowekwa na Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu vimeinyima Iran vyanzo muhimu vya kuiwezesha kulipa ada yake ya uanachama kwa Umoja wa Mataifa na sasa hivi inafanya mazungumzo ya wajibu wa kuondolewa vikwazo hivyo kwa ajili ya kutatua matatizo yaliyopo.

Msemaji huyo wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameongeza kuwa, hivi sasa pia juhudi za kweli zinafanyika kuhakikisha Tehran inalipa ada yake hiyo haraka iwezekanavyo.

Vile vile amesema, ni jukumu la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na sekretarieti ya umoja huo kutilia maanani mazingira maalumu ya nchi zilizowekewa vikwazo vya kidhulma na haramu kama ambavyo ni jukumu la umoja huo kutofautisha baina ya nchi zenye mazingira ya kawaida na zile zilizobebeshwa vikwazo vya kidhalimu na vilivyo kinyume cha sheria.

Duru mbalimbali za habari zimetangaza kuwa, nchi nane ikiwemo Iran zimesimamishiwa haki ya kupiga kura katika Umoja wa Mataifa kutokana na kutolipa ada zao za uanachama. Hayo ni matokeo mengine mabaya ya ugaidi wa kiuchumi wa Marekani dhidi ya Iran.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*