?>

Iran: Tuna nia ya kweli ya kushirikiana na wakala wa nyuklia wa IAEA

Iran: Tuna nia ya kweli ya kushirikiana na wakala wa nyuklia wa IAEA

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Tehran ina nia ya kweli ya kushirikiana na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Hossein Amir-Abdolahian alisema hayo jana Jumanne wakati alipoonana na Rafael Grossi, Mkurugenzi Mkuu wa IAEA na kusisitiza kuwa, nia ya Iran ni safi na kwamba Tehran ina azma ya kweli ya kushirikiana na wakala huo wa kimataifa wa nyuklia katika mipaka ya sheria zake. Amesema, ana matumaini safari ya Rafael Grossi hapa Iran itaimarisha zaidi uhusiano wa Tehran na IAEA.p

Vile vile Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ametilia mkazo umuhimu wa kufanywa mambo kiufundi na kiutaalamu, kutopendelea upande wowote Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki na kutokubali wakala huo kushinikizwa kisiasa na madola ya kigeni.

Kwa upande wake pia, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA amesisitizia umuhimu wa kufanyika mambo kiutalaamu na kiufundi na kutofanyika upendeleo wowote. 

Amesema, hatua yake ya kuitembelea Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni uthibitisho kuwa IAEA inalipa umuhimu suala la mazungumzo na kutatuliwa masuala yote yaliyopo kwa njia za kiufundi na kiutaalamu.

Aidha amesema, Wakala wa Kimataifa wa Niashati ya Atomiki nao unatilia mkazo kupatiwa ufumbuzi masuala yaliyobakia katika mazungumzo ya yanayohusiana na mapatano ya nyuklia ya JCPOA kama ambavyo inatilia mkazo pia kuendelea ushirikiano wa karibu baina yake na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.


342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*