?>

Iran: Tunapambana kishujaa na magenge ya watenda jinai

Iran: Tunapambana kishujaa na magenge ya watenda jinai

Mwakilishi wa kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu inafanya jitihada kubwa za kupambana na magenge yaliyojipanga vilivyo ya magendo ya binadamu na inaendesha mapambano hayo kishujaa licha ya kuwa chini ya vikwazo vya kidhalimu vya Marekani na kutoungwa mkono na jamii ya kimataifa.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Kwa mujibu wa shirika la habari la IRIB, Majid Takht-Ravanchi amesema hayo katika kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kilichozungumzia magendo ya wanadamu na kusisitiza kuwa, Iran ambayo ni moja ya nchi za kwanza kabisa kutia saini mkataba wa kimataifa wa kupambana na uhalifu wa magenge yaliyojipanga vilivyo, imechukua hatua zote za lazima za kutekeleza vipengee vya nyongeza mkataba huo katika kupambana na magendo ya wanadamu.

Vile vile amesema kuwa, Iran imeweka sheria nyingi za kuhakikisha wahalifu wote wanafuatiliwa kikamilifu na sheria na kusisitiza kuwa, Kamati ya Taifa ya Kukabiliana na Magendo ya Binadamu imeundwa chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Iran kwa ajili ya kusimamia na kuendesha mapambano dhidi ya magendo ya binadamu.

Mwakilishi huyo wa kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa vile vile amesema, Jamhuri ya Kiislamu inaihimiza jamii ya kimataifa iisaidie katika jitihada zake hizo za kishujaa ili vita dhidi ya magendo ya binadamu ambavyo vinahusu dunia nzima, viweze kufanyika kwa ufanisi mkubwa zaidi. 

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*